Kidato cha Tano hadi cha Sita

Kuanzishwa na Mahali Ilipo
Shule ya sekondari Maghabe inatoa elimu ya kidato cha tano hadi cha sita kuanzia mwaka 2015. Shule inapokea maombi ya kujiunga kidato cha tano kuanzia mwezi machi hadi mei kila mwaka. Shule ipo umbali wa kilomita 05 kutoka stendi ya Mbalizi na kilomita 17 kutoka stendi kuu ya mabasi Mbeya mjini.
Masomo yanayofundishwa
Shule ya sekondari Maghabe inafundisha masomo yafuatayo kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita:
- Mafunzo ya Jumla / Uraia (GS),
- Historia,
- Jiografia,
- Kingereza, na
- Kiswahili.
Tahasusi Zilizopo
Tahasusi zote zinajumuisha somo la mafunzo ya jumla kama somo la lazima. Tahasusi zinazofundishwa kwa sasa ni:
TAHASUSI MASOMO
HGL Historia, Jiografia, na Kingereza
HGK Historia, Jiografia, na Kiswahili
HKL Historia, Kiswahili, na Kingereza
Endapo umevutiwa na shule ya Maghabe na unahitaji kujiunga na masomo ya kidato cha tano na sita, kwa mwaka huu wa masomo, bobya hapa.
 
"The fear of the Lord is the source of Knowledge"
"Kumcha Bwana ni Chanzo cha Maarifa"
Maghabe Sekondari




© 2022 Shule ya Sekondari Maghabe, Mbeya. Haki zote zimehifadhiwa.