Udahili wa Wanafunzi

   Maelezo ya Kujiunga Kidato cha 5
   Maelezo ya Kujiunga Kidato cha 1
   Fomu ya maombi kujiunga kidato cha 5
    Fomu ya maombi kujiunga kidato cha 1
   Mwaliko kujiunge kidato cha 5, 2022
   Mwaliko kujiunge kidato cha 1, 2022
 
Udahili wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza
Shule ya sekondari Maghabe inapokea maombi ya kujiunga na kidato cha kwanza kuanzia mwezi Septemba hadi Novemba kila mwaka. Pia tuchapisha tangazo la kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka husika katika tovuti ya shule.
Mwanafunzi anayehitaji kujiunga kidato cha kwanza, Maghabe sekondari anatakiwa awe na sifa zifuatazo:
i.
Awe amehitimu kidato cha saba sio zaidi ya miaka mitatu kutoka mwaka anaoomba kujiunga kidato cha kwanza.
ii.
Awe amefaulu mtihani wa udahili (interview) unaotolewa na shule ya sekondari Maghabe.
iii.
Awe na umri usiopungua miaka 11.
iv.
Lazima akubaliane na sheria na kanuni za shule.
Shule ya sekondari Maghabe inapokea maombi ya kujiunga na kidato cha kwanza kuanzia mwezi Machi hadi Mei kila mwaka. Muda wa kuanza kutuma maombi na mwisho wa kupokea maombi utatangazwa kupitia tovuti ya shule.

Mwanafunzi anayehitaji kujiunga kidato cha tano, Maghabe sekondari anatakiwa awe na sifa zifuatazo:
i.
Awe amehitimu kidato cha saba sio zaidi ya miaka mitatu kutoka mwaka anaoomba kujiunga kidato cha tano.
ii.
Awe na angalau ufaulu wa alama "C" tatu katika Mtihani wa kidato cha nne (CSEE) alizozipata katika mtihani wa mwaka mmoja au miaka tofauti.
iii.
Lazima akubaliane na sheria na kanuni za shule.

Wanafunzi wanaweza kuomba kujiunga na shule kwa kujaza fomu zinazopatikana shuleni Maghabe, kwa mawakala au/na kupitia  tovuti ya shule.

Wakati wa kuomba nafasi mwanafunzi atatakiwa:

i.
Awe amekidhi vigezo au sifa za kujiunga na shule.
ii.
Kulipa ada ya maombi TZS 15,000 (kiasi hiki kinaweza kubadilika mwaka hadi mwaka).
iii.
Waombaji watakaochukua fomu kutoka shuleni Maghabe au kupitia wakala watalipa ada ya maombi kwa mtu aliyemkabidhi fomu, lakini waombaji watakaochukua fomu kupitia tovuti ya shule watalipa ada ya maombi kupitia akaunti ya benki.
iv.
Fomu zilizokwisha kujazwa zitarudishwa shuleni siku ya mtihani wa udahili kwa waombaji wa kidato cha kwanza, au tarehe itakayoelekezwa kwa wanafunzi wa kidato cha tano.
v.
Majina ya wanafunzi waliochaguliwa yatabandikwa katika kituo alichofanyia mtihani wa udahihi, shuleni na / au kuwekwa katika tovuti ya shule.
vi.
Wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga na shule watachukua fomu ya udahili, na sheria za shule kutoka shuleni maghabe au tovuti ya shule.
vii.
Mwanafunzi anatakiwa kuja shuleni na fomu ya udahili iliyosainiwa pamoja na sheria za shule siku ya udahili.

Udahili wa Wanafunzi wa Kidato cha Tano
Sifa za Kujiunga Kidato cha Tano
Namna ya Kuomba Nafasi za Masomo
Sifa za kujiunga kidato cha Kwanza
Pata Fomu ya Maombi ya Kujiunga

"The fear of the Lord is the source of Knowledge"
"Kumcha Bwana ni Chanzo cha Maarifa"
Maghabe Sekondari
© 2022 Shule ya Sekondari Maghabe, Mbeya. Haki zote zimehifadhiwa.